Staa wa muziki nchini Kenrazy ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha Sosuun na Dufla Diligion.
Rapa huyo mkongwe ametuweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushae picha ya pamoja na wasanii hao na kusindikiza na caption inayosomeka “SOSUUN x DUFLA DILIGON x KENRAZY Merry Christmas Everyone and STAY TUNED!!! LOADING…..”
Ujumbe huo unoshiria kuwa mashabiki wakae tayari kwa ajili ya mfululizo wa nyimbo kutoka kwa wakali hao ambazo huenda zikatoka hivi karibuni.
Ikumbukwe kazi ya mwisho iliyowaleta pamoja Kenrazy, Sosuun na Dufla Diligion ilikuwa ni wimbo uitwao Dawa ya moto ambao uliachiwa miaka 6 iliyopita chini ya lebo ya muziki ya Grapa Records