You are currently viewing KENRAZY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA KESHO

KENRAZY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA KESHO

Hatimaye nyota wa muziki nchini Kenrazy ameweka hadharani jina na cover rasmi la album yake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kenrazy ameshare artwork ya album yake mpya ambapo amesema album yake hiyo itaitwa Son of God.

Hitmaker huyo wa mbilikimo mkora amesema album yake mpya ina jumla ya mikwaju 20 za moto na itaingia sokoni oktoba 13 mwaka huu.

Album hiyo ilipaswa kutoka Septemba 27 mwaka lakini kenrazy aliahirishwa kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.

Hii itakuwa ni album ya tatu kutoka kwa mtu mzima kenrazy baada ya Ti-chi ya mwaka wa 2008 na Get it Right from Kenrazy ya mwaka wa 2011.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke