Msanii wa muziki nchini Kenzo Matata ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni.
Katika mahojiano na SPM Buzz Mkali huyo wa ngoma ya “Mama Milcah” ametusanua kuwa album yake mpya imekamilika ambapo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kuipokea.
Licha ya Kenzo Matata kutoweka wazi jina pamoja na idadi ngoma ya album yake mpya , amesema amewashirikisha wasanii mbali mbali kwenye album hiyo ambao kwa mujibu wake wanatoka tanzania, uganda, Ujerumani na Kenya.
Hii itakuwa ni album ya kwanza kwa mtu Kenzo Matata tangu aanze safari yake muziki mapema miaka ya 2000 akiwa chini lebo ya muziki ya Ogopa Deejays.