Rapa kutoka Marekani Cardi B yuko hatarini kufungwa miaka minne jela kufuatia mashtaka mawili yanayomkabili,ya kuwapiga na kuwafanyia fujo wahudumu wawili wa club iitwayo Angels-Strip-Club
Mwaka 2018 Cardi B alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa makosa hayo mawili lakini mwaka wa 2019 alikanusha kwenye mahakama kuu ya queens akiwa kizimbani kwa kumwambia hakimu kuwa hana hatia
Inadaiwa Cardi B alitoa maelekezo kwa wasaidizi wake kuwapiga wahudumu hao wawili wa klabu hiyo na baadaye yeye pia alishiriki kutembeza kipigo, kurusha viti na kupasua chupa mara baada ya kusikia kuwa mmoja kati yao alitoka kimapenzi na mumewe Offset.
Hata hivyo usikilizaji wa kesi hiyo umepangwa kufanya oktoba 25, mwaka huu na endapo rapa huyo atakutwa na hatia ya makosa yote mawili basi kifungo cha miaka minne jela kitamhusu