Rapa Kanye West hatashitakiwa kwa kumpiga ngumi shabiki mmoja ambaye alikuja kwa ajili ya kutaka kupiga picha nae, mwezi Januari mwaka huu.
Tukio hilo lilitokea Jijini Los Angeles ambapo shabiki huyo alidai kwamba baada ya kumuomba YE kupiga nae picha, walijikuta wakijibazana na ghafla rapa huyo alishuka kwenye gari na kumpiga ngumi mbili, moja kichwani na nyingine shingoni ambapo alianguka chini.
Idara ya Polisi imechunguza shauri hilo ambalo linabeba hukumu ya miezi 6 Jela, na taarifa mpya ni kuwa wamekuta hakuna ushahidi wa kutosha kumtia hatiani Kanye West.