Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Tyga hatashtakiwa kwa makosa ya jinai katika kesi yake ya unyanyasaji wa nyumbani dhidi ya mpenzi wake wa zamani Camaryn Swanson.
Mapema wiki hii TMZ imeripoti kwamba kesi ya Tyga itasikilizwa katika Ofisi ya Mwanasheria wa Jiji la Los Angeles, ambapo atajadili jinsi ya kushughulikia migogoro ya nyumbani.
Hapo awali, iliripotiwa kuwa Tyga bado anaweza kushtakiwa kwa kosa la kumpiga makonde mpenzi wake wa zamani Camaryn Swanson kutokana na madai ya ugomvi kati yake na mpenzi wake Huyo uliotokea Oktoba Mwaka Jana.