Rapa Khaligraph Jones amewapa mashabiki wake orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya “Invisible Currency” (Sarafu isiyoonekana) anayoitarajia kuitoa hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa instagram ameachia tracklist ya album yake hiyo mpya ambapo ina jumla ya nyimbo 17 huku ikiwa na collabo 10 pekee.
Hitmaker huyo wa “Luku” amewapa mashavu wakali kama Alikiba, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi.
Invisible Currency itakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones baada ya “Testimony 1990” ya mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17.