You are currently viewing KHALIGRAPH JONES AANDIKA BARUA YA WAZI KWA RUTO KUPITIA WIMBO

KHALIGRAPH JONES AANDIKA BARUA YA WAZI KWA RUTO KUPITIA WIMBO

Rapper Brian Omollo maarufu kama Khaligraph Jones, amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kumuandikia barua ya wazi rais mteule william ruto kupitia singo yake mpya iitwayo “Usiache Akemewe Free style”

Kupitia wimbo huo rapa huyo ametoa wito kwa Ruto kuweka kipau mbele suala la kuwaleta wakenya pamoja pindi atakapoapishwa rasmi kuitumikia Kenya kwa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wakenya.

Khaligraph Jones ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna baadhi ya watu wanamshambulia kiongozi wa Azimio Raila Odinga bila kujua kwamba matusi yao inamkosesha amani huku akisema kuwa anafahamu kuwa Ruto ambaye ni mcha mungu ana uwezo wa kumaliza uhasama wa kisiasa unaoshuhudia kwa sasa nchini.

Papa Jones amefichua kuwa mama yake amekuwa mgonjwa tangu Raila apoteze uchaguzi uliokamilika lakini Ruto akimpa heshima kiongozi huyo mama yake pamoja na wafuasi wengine wa azimio wanaopitia wakati mgumu mioyoni mwao watafarijika.

Hata hivyo amemalizia wimbo huo wa dakika 2 sekunde 6 kwa kumpongeza Rais Mteule William Ruto kwa mara nyingine huku akimshukuru kwa kumsikiliza.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke