Aliyekuwa mpenzi wa msanii Khaligraph Jones,Cashy ameshambulia mwanamuziki huyo akidai kuwa amhudumii mtoto wake wa kiume aliyezaa naye mwaka wa 2018 pindi tu walipoachana.
Cashy ameshukuru kufunguliwa kwa nchi ambapo amesema kuwa itakuwa afueni kwa wasanii kupata angalau matamasha ya kuwaingizia pesa kwani wengi wao walikuwa wanategemea matamasha kupata riziki.
Kutokana na hilo amesema Papa Jones hatakuwa na sababu zingine za kuepuka majukumu ya kumlea mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu kwa sasa ikizingatiwa kuwa tangu ujio wa Corona rapa huyo amekuwa akidai kuwa hakuwa na pesa za kumhudumia mwanae.
Hata hivyo khalighraph jones hajetoa tamko kuhusiana na madai yaliyoibuliwa na baby mama wake kuwa amemtelekeza mtoto wake