You are currently viewing KHALIGRAPH JONES AHIRISHA KUACHIWA KWA VIDEO YA MAOMBI YA MAMA KISA MSIBA WA MWAI KIBAKI

KHALIGRAPH JONES AHIRISHA KUACHIWA KWA VIDEO YA MAOMBI YA MAMA KISA MSIBA WA MWAI KIBAKI

Rapa Khaligraph Jones ameahirisha kuachia video ya wimbo wake uliokuwa ukisubiriwana mashabiki uitwao ‘Maombi ya Mama’ kwa ajili ya kumuenzi Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki aliyefariki mwishoni mwa juma lilopitwa.

Kupitia ukurasa wake wa instagram bosi huyo wa Blue Ink, amesema video hiyo ilipaswa kuachia rasmi wiki lakini italazimika kusubiri hadi marehemu rais mwai kibaki atakapozikwa.

Maombi ya Mama ni wimbo namba 7 kutoka kwenye albamu yake Invisible Currency na ni wimbo ambao amemshirikisha msanii wa kike nchini Adasa.

Wengine walioshirikishwa kwenye Albamu ya Khaligraph Jones ni pamoja na; Alikiba, Prince Indah, Mejja, Blackway, Rudeboy, Kev the Topic, Scar, Xenia Manasseh, na Dax.

Album ya “Invisible Currency” iliachiwa rasmi Machi 7 mwaka 2022 ikiwa na jumla ya ngoma 17 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima  Khaligraph Jones  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Testimony 1990 iliyotoka mwaka 2018.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke