You are currently viewing KHALIGRAPH JONES ALALAMIKIA KUPANDA KWA GHARAMA YA MAISHA

KHALIGRAPH JONES ALALAMIKIA KUPANDA KWA GHARAMA YA MAISHA

Rapa Khaligraph Jones ameonekana kulemewa na shughuli za ujenzi wa nyumba yake ya kifahari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Papa Jones amelalamika kupanda kwa gharama ya vifaa vya ujenzi nchini huku akitoa wito kwa serikali kuingia kati na kushusha bei ya vifaa hivyo kama njia moja ya kuwasaidia wakenya wa kawaida kukamilisha miradi yao.

“Sirkali Saidia, Bei Ya Chuma ya Kujenga imepanda kuliko Iphone 13 pro Max, Sikuizi Kwa nyumba Beef tunakula once a week, kama leo Usiku ni Ugali na mboga tu. #respecttheogs“, Ameandika kupitia Instastory yake.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumtolea uvivu rapa huyo kwa kuwakejeli wakenya ambao wanaishi maisha ya uchochole kwa kujaribu kuonesha namna ambavyo analamimikia vitu vya starehe.

Utakumbuka juzi kati Khaligraph Jones alishare kupitia Instagram yake maendeleo ya mjengo wake wa kifahari ambao amekuwa akiujenga.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke