You are currently viewing KHALIGRAPH JONES ASHINDWA KUFICHA UPENDO WAKE KWA KRISTOFF, AMTAKA RAPA HUYO ARUDI KWENYE MUZIKI

KHALIGRAPH JONES ASHINDWA KUFICHA UPENDO WAKE KWA KRISTOFF, AMTAKA RAPA HUYO ARUDI KWENYE MUZIKI

Rapa Khaligraph Jones ameshindwa kuvumlia ukimya  wa rapa mwenzake Kristoff ambaye amepotea kwenye tasnia ya muziki nchini kwa muda sasa bila kuachia kazi yeyote.

Kupitia Instagram page yake Papa Jones amepost clip fupi ya rapa huyo akichana kwenye wimbo wa “We be happening remix” na kusema kwamba ameshangazwa na kilichomsibu Kristoff akapotea ghafla kwenye muziki wake kwani alikuwa mmoja wa marapa wakali nchini.

Hitmaker huyo wa “Champez” ametoa changamoto kwa Kristoff ajikakamua mwaka huu ili aweze kurudi kwenye tasnia ya muziki nchini ikizingatiwa  bado mashabiki wanamhitaji kutokana na kipaji chake cha kurap kwenye muziki wa hihop.

Hata hivyo mastaa wengi wa muziki nchini na mashabiki wameonekana kumuunga mkono khaligraph jones wakimtaka kristoff arudi kwenye muziki wa hiphop kwani ana uwezo mkubwa wa kuupeleka muziki wake kimataifa.

Hajabainika sababu zilizompelekea khaligraph jones kumpost kristoff ila walimwengu wanahoji kuwa huenda wawili hao wana wimbo wa pamoja ambao wana mpango wa kuuachia hivi karibuni.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma wawili hao waliachia ngoma kali kama We be happening, Biashara wakiwa na Stella Mwangi, Fly na nyingine kibao

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke