You are currently viewing KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA KUWAHI KUTAKA KUACHA MUZIKI.

KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA KUWAHI KUTAKA KUACHA MUZIKI.

Rapa Khaligraph Jones ametusanua kuhusu changamoto alizokutana  nazo katika safari yake ya muziki ambayo ilimpelekea kutaka kuchukua maamuzi magumu kwenye maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa instagram amepost picha akiwa jukwaani katika chuo kikuu cha St. Pauls limuru mwaka wa 2012 na kusema kwamba mashabiki waliikata perfomance yake na kumtimua jukwaani jambo ambalo lilimfanya kufikiria kuacha muziki.

Lakini baada ya kujitafakari upya na kuweka bidii kwenye kazi zake za muziki aliweza kuwaaminisha watu waliombeza kipindi hicho kwamba anaweza kwenye tasnia ya muziki nchini.

Khalighraph jones ni moja kati ya marapa maarufu barani afrika na licha ya kutimuliwa jukwanii mwaka wa 2012 nchini Kenya ametumbuiza kwenye majukwaa makubwa ya muziki duniani lakini pia ameshinda tuzo kadhaa za muziki ikiwemo B.E.T na Sound city Africa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke