Rapa Khaligraph Jones ametoa changamoto kwa wasanii wa muziki wa Gengetone waache kulalamika juu ya kukosa usimamizi.
Rapa huyo amewataka wasanii hao, kutotumia silaha ya kukosa uongozi kama chanzo cha wao kushindwa kufanya muziki na badala yake wajifunze kutoa kazi zao wenyewe bila kutegemea lebo za muziki ambazo muda mwingine huwapoteza kimuziki.
Katika hatua nyingine, ameamua kuweka wazi kuhusu taarifa za muda mrefu zilizosambaa kuwa hana maelewano mazuri na rapa mwenzake Octopizo.
Papa Jones amesema hana ugomvi au mkwaruzano wowote na rapa huyo kwani watu ndio wamekuwa wakiwaingiza kwenye matatizo.