You are currently viewing KHALIGRAPH JONES AWAPA WANASIASA RUHUSA YA KUTUMIA NYIMBO ZAKE

KHALIGRAPH JONES AWAPA WANASIASA RUHUSA YA KUTUMIA NYIMBO ZAKE

Rapa Khaligraph Jones amewapa wanasiasa ruhusa ya kucheza nyimbo zake bila malipo kwenye shughuli zao za kisiasa.

Katika mahojiano na Ramogi Tv Mkali huyo wa ngoma ya ‘Mazishi’ amesema hatamfungulia mtu yeyote kesi mahakamani kwa kutumia kazi zake za muziki bila idhini yake.

“Cheza tu muziki wangu unapoweza, sitampeleka mtu yeyote mahakamani kwa hilo,” alisema.

Kauli yake imekuja siku chache baada ya Sauti Sol kutishia kuuchukulia muungano wa Azimio hatua kali za kisheria kwa kucheza muziki wao bila kibali.

Sauti Sol, kupitia taarifa walidai kulipwa fidia, ambapo tuliona member wa kundi hilo Bien akisema kuwa wanatarajia kulipwa pesa nyingi.

Hata hivyo, sio wanachama wote wa Sauti Sol walikuwa wanaunga mkono hatua hiyo, kwani Savara alijitokeza wazi na kudai  kuwa hana shida yeyote kwa nyimbo zake zikichezwa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke