You are currently viewing KHALIGRAPH JONES AWEKA WAZI MWEZI AMBAO ALBUM YAKE MPYA ITAINGIA SOKONI

KHALIGRAPH JONES AWEKA WAZI MWEZI AMBAO ALBUM YAKE MPYA ITAINGIA SOKONI

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khaligraph Jones anaendelea kutupasha mapya kuhusu ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni.

Kwenye mkao na wanahabari Papa Jones amesema album yake “Invisble Currency” itaingia rasmi sokoni mwezi Disemba mwaka huu ingawa hajaweka wazi tarehe rasmi ambayo  ataachia album yake hiyo.

Tayari Papa Jones tayari ameachia rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya “Invisible Currency” ambayo ina jumla ya nyimbo 17 huku ikiwa na collabo 10 pekee.

Hitmaker huyo wa “Luku” amewapa mashavu wakali kama Ali Kiba, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi.

Invisible Currency itakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones baada ya “Testimony 1990” ya mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17.

Kauli ya Khaligraph Jones baada ya kuingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya Galactic Kenya ambayo inajihusisha na biashara ya kuuza vifaa vya magari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke