You are currently viewing KHALIGRAPH JONES NA KING KAKA WAOMBOLEZA KIFO CHA RAPA RIKY RICK KUTOKA AFRIKA KUSINI

KHALIGRAPH JONES NA KING KAKA WAOMBOLEZA KIFO CHA RAPA RIKY RICK KUTOKA AFRIKA KUSINI

Rapa Khaligraph Jones ameungana na wapenzi wa muziki wa hiphop Barani Afrika kumuomboleza kifo cha rapa riky Rick ambaye alifariki februari 23 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones ameshare screen shot ya mazungumzo ya siri kati yake na rapa huyo ambapo amesema kuwa mwaka wa 2018 alikuwa na matamanio ya kufanya kazi ya pamoja na riky rick lakini hakufanikisha suala hilo kutokana na ugumu wa kumfikia.

Kwa upande wake Rapa King Kaka amesema walikutana na Riky Rick miaka kadhaa iliyopita nchini ufaransa kwenye moja ya party ambapo alipata wasaa mzuri kubadilishana mawazo na rapa huyo ambaye kwa mujibu wake alikuwa mtu mkarimu zaidi kuwahi kukutana naye.

Riky Rick alifariki dunia februari 23 mwaka huu baada ya kujitoa uhai nyumbani kwake kaskazini mwa Joburg Jumatano asubuhi.

Chanzo cha Kifo chake hakijatajwa lakini baadhi ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vinaripoti kwamba Riky Rick alijinyonga baada ya kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Rapa huyo alianza kujipatia umaarufu mwaka 2015 kupitia ngoma yake iitwayo, Boss Zonke.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke