You are currently viewing Khaligraph Jones na wasanii wengine kutoka Kenya watajwa kuwania tuzo za Sound City MVP 2023

Khaligraph Jones na wasanii wengine kutoka Kenya watajwa kuwania tuzo za Sound City MVP 2023

Kituo cha Televisheni cha Sound City kimeanika vipengele vya Tuzo zake za Sound City MVP 2023 ambapo wasanii mbali mbali kutoka barani Afrika wametajwa kuwania Tuzo hizo kwa mwaka huu zinazotarajiwa kutolewa Februari 11.

Kenya imepata Vipengele kadhaa ambapo tumewakilishwa na Khaligraph Jones, Wakadinali, Bien, pamoja na Aaron Rimbui.

Khaligraph Jones ametajwa kwenye kipengele cha Best Hiphop. Wakadinali nao wametajwa kwenye kipengele hicho.

Bien wa Sauti Sol ametajwa kuwania Tuzo ya “Song of the Year” kupitia wimbo wake na Aaron Rimbui uitwao “Mbwebwe.

Kundi la Wakadinali wanaipeperusha bendera ya Kenya upande wa Kipengele cha “Best New MVP” ambapo atachuana na wakali kama Phina, Ayra Starr, Costa Titch, Black Sherif na wengine wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke