Kijana aliyesukumwa stejini na Burna Boy ameahidi kutovua shati mwaka mzima, shati ambalo alilivaa usiku ule aliosukumwa wakati akijaribu kuomba msaada kwa Staa huyo wa muziki kutoka nchini Nigeria.
Kwenye mahojiano na vyombo vya habari nchini Nigeria kijana huyo amesema ni fahari sana kwake na alifurahishwa na lile tukio ndio maana ameapa kulitunza mwilini shati hilo mwaka mzima.
Lakini pia amekiri mapenzi yake kwa Burna Boy ni makubwa sana na anamuomba msaada na wasanii wengine wa Nigeria wamsaidie kwani ana kipaji cha kuimba.