You are currently viewing KILLY AWAOMBA MASHABIKI WA KENYA WAMSAIDIE KUPATA ALIYEONDOA VIDEO YA WIMBO WAKE YOUTUBE

KILLY AWAOMBA MASHABIKI WA KENYA WAMSAIDIE KUPATA ALIYEONDOA VIDEO YA WIMBO WAKE YOUTUBE

Msanii wa Bongofleva, Killy amewaomba mashabiki wake waliyopo nchini Kenya kumsaidia kumpata Mutisya Munyithya ambaye ndiye ameipiga copy right YouTube video ya wimbo wake, Ni Yeye ambao amemshirikisha Harmonize.

Mwimbaji huyo wa Konde Music Worldwide amewaomba mashabiki wanaomfahamu wawasiliane naye kwa namba +255 65 289 2317.

“Mashabiki zangu pendwa poleni sana kwa maumivu ya kuondolewa kwa video yetu pendwa ya Ni Wewe. Hii ni moja ya changamoto tu katika kazi zetu japo inaumiza sana ila hatuna budi kuwa na subira”.

“Ni changamoto ambayo ipo nje wa uwezo wangu ila Menejimenti ina shughulikia hilo na video yetu Ni Wewe itarudi tu soon, love you all my fans” amesema Killy.

Hadi inaondolewa YouTube video hiyo ilikuwa na views zaidi ya milioni 2.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke