Nyota wa muziki wa bongofleva Killy ametangaza kuja na Extended Playlist ‘EP’ yake ,aliyoipa jina la ‘The Green Light ‘ inayotarajiwa kutoka ndani ya mwaka huu.
Kupitia ukurasa wa instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya ‘Ni Wewe’ amesema ‘EP’ hiyo ina jumla ya nyimbo 5 ,huku akiwa amewashirikisha wasanii wawili ambao ni ibraah kutoka Konde Gang na Christian bella.
Pamoja na kutangaza ujio wa EP hiyo Killy hajaweka wazi ni lini EP hiyo itatoka rasmi.
Mpaka sasa mwanamuziki huyo anashikilia nafasi ya kwanza katika trending tab za mtandao wa YouTube nchini tanzania kupitia wimbo wake wa Ni wewe’ ambayo ina jumla ya views million 1.8.