You are currently viewing KIM KARDASHIAN ADAI TALAKA LICHA YA KANYE WEST KUMHITAJI

KIM KARDASHIAN ADAI TALAKA LICHA YA KANYE WEST KUMHITAJI

Kim Kardashian bado anaitaka talaka yake licha ya harakati za Kanye West ambaye anapambana ili ndoa yake isivunjike.

Sasa wakati mchakato wa talaka ukiwa bado unaendelea mahakamani, Kim anaonekana anataka kuwa huru na maisha yake kwa wakati huu.

Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba jana Ijumaa Kim Kardashian alijaza nyaraka za kisheria akitaka kuwa ‘single’ yaani mwanamke asiye na mpenzi. Pia ameenda mbali zaidi na kutaka kuondolewa kwa jina la ‘WEST’ mwishoni mwa majina yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke