You are currently viewing KIM KARDASHIAN AMPA MASHAVU KAMA YOTE KANYE WEST, AMUITA RAPA MKALI WA MUDA WOTE.

KIM KARDASHIAN AMPA MASHAVU KAMA YOTE KANYE WEST, AMUITA RAPA MKALI WA MUDA WOTE.

Kim Kardashian alikuwa Host wa kipindi cha Saturday Night Live (SNL) wikendi hii iliyomalizika ikiwa ni kwa mara ya kwanza.

Mengi makubwa yalifanyika na kuwafurahisha watazamaji wa kipindi hicho lakini maneno ya Kim kuhusu Kanye  West yaliwavutia wengi zaidi.

Kwenye maneno ya ufunguzi wa kipindi hicho, Kim alizungumzia mumewe Kanye West pamoja na familia yake kwa ujumla

“Niliolewa na Rapa mkali wa muda wote. Si hivyo tu, ni Mtu mweusi Tajiri zaidi nchini Marekani. Mtu mwenye kipaji cha aina yake mwenye fikra (genius) ambaye amenipatia watoto wanne wazuri.” alisema Kim Kardashian.

Wawili hao wanaendelea kutuweka njia panda kufuatia sakata la talaka ambalo linaendelea baina yao, kwani walionekana wakiondoka hotelini pamoja mjini New York masaa machache kabla ya Saturday Night Live kuanza.

Kim pia amekuwa karibu na Kanye West kipindi chote cha uzinduzi wa album ya DONDA.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke