You are currently viewing KIM KARDASHIAN ASHINDA KIPENGELE CHA UMILIKI WA NYUMBA KWENYE SHAURI LA TALAKA

KIM KARDASHIAN ASHINDA KIPENGELE CHA UMILIKI WA NYUMBA KWENYE SHAURI LA TALAKA

Mahakama ya mjini Los angeles nchini marekani imempatia ushindi Kim Kardashian wa umiliki wa nyumba kwenye shauri la talaka linaloendelea dhidi yaKkanye West.

Kim ameshinda kipengele hicho na sasa ni mmiliki wa nyumba ambayo walianzia maisha na Kanye West na kuanzisha familia pamoja.

Jumba hilo lenye thamani ya shilling billion 6.7  lipo mjini Hidden Hills California, mwaka wa 2014 walilinunua pamoja kwa shilling billioni 2.6 kisha baadaye mwaka wa 2020 Kanye West aliikarabati.

Hii imekuja kufuatia mustakabali wa watoto wao ambao wamezoea kuishi mahali hapo.

Taarifa hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu kanye west aiweke kwenye mnada moja ya ranchi zake zilizopo huko Wyoming nchini kwa shilling billioni 1.2.

Mwezi uliopita  Kanye West pia aliripotiwa kununua jumba la kifahari kwenye fukwe za malibu huko marekani kwa shilling billioni 6.3.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke