Baby Mama wa Rapa Kanye West, Kim Kardashian ameripotiwa kupokea vitisho vya bomu na kifo kutoka kwa mtu asiyejulikana.
Kwa mujibu wa TMZ, Kim anadai kuwa maisha yake pamoja na watoto wake yapo hatarini, hii ni baada ya kupokea barua kadhaa zinazotishia kuondoa uhai wake, ambapo mwandishi wa barua hizo ametishia kulipua ofisi ya Kim kwa bomu.
Kim amedai kupata barua kutoka kwa jamaa anayefahamika kama David Resindez, ambaye ana anuani zake za nyumbani na biashara, na tayari ameshatuma barua zaidi ya 80 za kumtishia yeye pamoja na watoto wake wa nne.
Hata hivyo, mwanasheria wa Kim, Shawn Holley anatajwa tayari kufanya utaratibu wa kupata zuio la mahakama juu ya mtu huyo kutoendelea kutoa vitisho hivyo.