Mkali wa muziki wa Hiphop nchini King Kaka ameachia rasmi Cover ya EP yake ijayo iinayokwenda kwa jina la “Happy Hour”
Kupitia ukurasa wake instagram King Kaka ametuonyesha cover ya EP yake mpya huku akiwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea EP hiyo.
Licha ya kuweka wazi jina na cover ya album yake mpya, King Kaka hajatuambia idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye EP hiyo ilia inatarajiwa kuingia sokoni Novemba 30 mwaka huu.
Ikumbukwe Happy Hour EP kutoka kwa mtu mzima King Kaka ilipaswa kuachiwa rasmi Oktoba mosi mwaka huu lakini ilishindikana kutokana na King Kaka kujikita kwenye kuiweka sawa afya yake baada ya kuugua kwa kipindi cha miezi minne iliyopita.