You are currently viewing KING KAKA AACHIA RASMI EP YAKE MPYA “HAPPY HOUR”

KING KAKA AACHIA RASMI EP YAKE MPYA “HAPPY HOUR”

Hatimaye rapa King Kaka amekata kiu ya mashabiki zake na EP mpya inayokwenda kwa jina la Happy Hour EP.

King Kaka ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia EP hiyo mpya yenye jumla ya mikwaju 11 ya moto huku ikiwa na kolabo 7 ambazo amewashirikisha wakali kama Ykee Benda, Kristoff, Wakadinali, Rich Mavoko, Amos and Josh na wengine wengine.

Happy Hour EP ina nyimbo kama Get Paid, Noma, Ingine, Kuzitoka, Mali safi na nyingine kibao.

Hata hivyo King Kaka amesema ameachia Happy Hour EP kama njia ya kumshukuru Mungu kwa uhai aliyompa baada ya kuugua kwa kipindi cha miezi mitatu.

Hii ni kazi ya pili  kwa mtu mzima King Kaka baada ya mixtape yake “The Servant and The King” ya mwaka wa 2016 na inapatikana exclusive kwenye Digital Platforms zote za kusambaza muziki duniani ikiwemo Boomplay.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke