Rapa King Kaka amelamba dili nono la kuwa balozi wa kampuni ya Simu ya Itel kwa upande wa Kenya.
King Kaka ametangaza habari njema kwa wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kubwa kujiunga na familia ya Itel inayojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki
“Mabibi na Mabwana, leo ni siku KUBWA SANA. Sasa unamtazama BALOZI MPYA wa @itelkenya @itelhome_kenya. Utukufu wote kwa Mungu. Ushindi kwa vijana wa Ghetto ambao wana imani, Ushindi kwa wabunifu, Ushindi kwa watumiaji wa Itel na Ushindi kwa Kenya!!! #KakaEmpireIsTheLifestyle.” King Kaka ameandika
Kwa upande wao Itel Kenya wameeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha King Kaka kuwa balozi wa kampuni hiyo kwa kuwa wana Imani rapa huyo atatumia ushawishi wake kwenye jamii kuwafikishia wateja wao bidhaa zao za simu.
“Tunayofuraha kutangaza ushirikiano na King Kaka. Anaakisi maadili ya matumizi mengi, ukamilifu na uvumbuzi ambayo tunafuata kwa uthabiti katika itel. Karibu kwa familia ya itel” Kampuni ya itel imeandika Instagram
King Kaka sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za itel kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.