You are currently viewing KING KAKA AMJENGEA MAMA YAKE MZAZI MJENGO WA KIFAHARI

KING KAKA AMJENGEA MAMA YAKE MZAZI MJENGO WA KIFAHARI

Rapa wa Kenya King Kaka anazidi Kujipakulia Baraka Za Wazazi wake,hii ni baada ya kumjengea mamake mzazi mjengo wa kifahari.

Kusindikiza taarifa hiyo, King Kaka amesimulia kisa kimoja ambacho kilimsukuma kutafuta hela ili kuja kumsaidia mama yake.

“Siku moja nilifika nyumbani nikitoka shule, Askari wa Jiji alikuwa alikuwa ameweka kufuli kubwa sana mlangoni kwetu kwa sababu tulishindwa kulipa Kodi ya nyumba ya shilling 500. Nilimuahidi Mama yangu kwamba baadaye nitakuja kumnunulia nyumba. Sasa siku Nne zilizopita, tulifanya maombi tukiwa kwenye sebule ya nyumba hii ambayo nimemjengea.” ameandika King Kaka.

Ni post ambayo imeshabikiwa na wafuasi wake kwenye mtandao wa instagram wakimpongeza kwa hatua ya kuwafanyia wazazi wake vitu vikubwa ambavyo vijana wengi wameshindwa kufanya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke