You are currently viewing KING KAKA ASAINI DILI LA USHIRIKIANO NA JUKWAA LA MTANDAONI LA AFYA REKOD

KING KAKA ASAINI DILI LA USHIRIKIANO NA JUKWAA LA MTANDAONI LA AFYA REKOD

Hakika huu ni mwaka wa Neema kwa rapa kutoka Kenya King Kaka, hii ni baada ya kutangaza kuingia ubia wa kufanya kazi na jukwaa la kuto huduma za kimatibabu kwa njia ya kidijitali, Afya Rekod.

Kupitia mitandao yake ya kijamii King Kaka amesema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuendeleza ukuaji wa matibabu wa kidijitali nchini na hata kuwapunguzia wagojwa mzigo wa kusafiri kutafuta matibabu.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Fight” amesema  ushirikiano huo pia unalenga kuhamasisha umma kuhusu matibabu kupitia mfumo wa kidijitali huku akisema kuna haja kwa hospitali au vituo vya afya kukumbatia mfumo wa kidijitali hasa katika kufuatilia hali ya wagonjwa waliolazwa.

Kampuni ya Afya Rekod inajishughulisha na masuala ya kuhifadhi maelezo ya kibinafsi ya mgonjwa, taarifa kamili kuhusu aina ya ugonjwa anayougua mhusika kwa njia ya mtandao.

Huduma zinazotolewa kupitia programu hizo ni upendekezaji wa tiba na ushirikiano na mawasiliano ya karibu kati ya mgonjwa na daktari wake.

King Kaka ni mmoja wa mastaa wa humu nchini ambao kati siku za hivi karibu wamepata ubalozi wa makampuni mbali mbali kutokana na ushawishi wao mkubwa kwenye jamii, wiki kadhaa zilizopata alilamba dili nono la kuwa balozi wa  kampuni ya simu ya mkononi ya Itel.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke