Rapa kutoka nchini Kenya, King Kaka ametangaza rasmi kuwa kuanzia sasa atakuwa anashabikia timu ya Arsenal baada ya kuachana na Manchester United.
King Kaka ambaye kwa miaka mingi amekuwa akishabikia Manchester United ameeleza kutoridhishwa kwake na matokeo ya timu hiyo kwa michezo ya hivi karibuni.
“Nadhani ni wakati sahihi nianze kutafuta raha kwingineko, ni rasmi kwamba sasa nashabikia Arsenal,” amesema King Kaka.
Utakumbuka hatua hii ya King Kaka inakuja muda mfupi baada ya Manchester United kulazwa magoli manne kwa moja na majirani wao Manchester City, huku Arsenal wakipata ushindi wa magoli matatu kwa mawili ugenini dhidi ya Watford.