You are currently viewing KING KAKA ATANGAZA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

KING KAKA ATANGAZA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

Rapper kutoka Nchini Kenya King Kaka ametusanua kuwa album yake mpya imekamilika.

Mkali huyo wa ngoma ya “Fight” ameweka wazi hilo kwenye podcast ya jalang’o tv huku akiwataka Mashabiki zake wakae Mkao Wa Kuipokea Album Yake Mpya Itakayoingia Sokoni Hivi Karibuni.

Hata hivyo King Kaka hajatuambia idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album hiyo wala tarehe rasmi ya album yenyewe kuingia sokoni ila ni jambo la kusubiriwa

Hii itakuwa ni album ya sita kwa mtu mzima wa King Kaka tangu aanze safari yake muziki ikizingatiwa kuwa tayari ana album tano, mixtape 9 na EP moja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke