You are currently viewing KING KAKA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI NCHINI MAREKANI

KING KAKA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI NCHINI MAREKANI

Rapa King Kaka ametangaza ujio wa ziara yake ya muziki  nchini marekani  kwa kuanika mkeka wa miji ambayo atafanya shows zake.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram king kaka, ameipa ziara hiyo jina la  Coast To Coast Summer 2022  USA  Tour ambapo amesema itafanyika ndani ya miji 13.

Ziara hiyo ambayo anafanya kwa ushirikiano na Rarequest Music Group inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Boston, Chicago, Minnesota, Atlanta, Dallas, na Los Angeles.

Hata hivyo hajaweka tarehe na mwezi ambayo ataanza tour yake hiyo ila king kaka amewataka mashabiki zake kufuatilia mitandao yake ya kijamii kwani yupo mbioni kuweka mambo sawa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke