Rapa King Kaka ameweka wazi tarehe ambayo EP yake mpya iitwayo Happy Hour itaingia sokoni.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter King Kaka amesema Happy Hour EP itatoka rasmi Novemba 30 mwaka huu ingawa hajaweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye EP hiyo.
Hitmaker wa “Fight” amesema singo ya kwanza kutoka kwenye EP yake ya Happy Hour ambayo wawashirikisha wasanii wa kundi la Wakadinali itaachia muda wowote kuanzia sasa.
Ikumbukwe Happy Hour EP kutoka kwa mtu mzima King Kaka ilipaswa kuachiwa rasmi Oktoba mosi mwaka huu lakini ilishindikana kutokana na rapa huyo kujikita kwenye kuiweka sawa afya yake baada ya kuugua kwa kipindi cha miezi mitatu.