Msanii wa muziki wa dancehall kutoka nchini Uganda King Michael amepewa adhabu ya kufanya usafi katika mahakama ya Makindye mara baada ya kuachiwa uhuru mapema wiki hii.
King Michael alikamatwa na maafisa usalama mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kosa la kukiuka kanuni za kuthibiti msambao wa Corona ambapo alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu, Novemba 8.
Baada ya King Michael kukiri makosa yake, Hakimu katika mahakama ya Makindye alimpa kifungo cha nje na kumuagiza afanye shughuli ya usafi katika mahakama hiyo kwa kipindi cha wiki moja.
Hata hivyo King Michael atatakiwa kuzoa taka, kufyeka vichaka, kuziba mitaro ya maji taka hadi pale kifungo chake cha nje kitakapokamilika