Msanii nyota kutoka Uganda King Saha amefunguka na kudai kwamba yuko tayari kufanya kazi na serikali ya nchini hiyo iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa muungano wa Wanamuziki nchini uganda (UMA).
Mkali huyo wa ngoma ya “Sivaawo” ameeleza katika mahojiano ya hivi karibuni kuwa ili muungano huo unufaike ni lazima uongozi wa UMA ushirikiane na watekelezaji wa sera.
King Saha amesema ana uhakika kwamba uhusiano mzuri na serikali utaleta manufaa kwenye tasnia ya muziki nchini uganda.
“Nitashirikiana na kila mtu ana nia njema ya kuboresha tasnia yaa muziki, hata serikali kwa sababu wao ndio watunga sera. Tunahitaji serikali ijumuishe kila mtu katika tasnia sio watu wachache tu,” alisema kwenye mahojiano na YouTuber mmoja mwishoni mwa juma lilopita .
Utakumbuka King Saha anatarajiwa kupambana na rais wa sasa wa muungano wa wasanii nchini Uganda Cindy Sanyu kwenye uchaguzi wa muungano huo ambao utafanyika hivi karibuni.