You are currently viewing KING SAHA AFUNGUKA KUPATA SHINIKIZO ZA KUJIUNGA NA SIASA

KING SAHA AFUNGUKA KUPATA SHINIKIZO ZA KUJIUNGA NA SIASA

Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha amefichua kuwa watu wake wa karibu wameanza kumpa shinikizo za kujiunga na siasa.

Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema “Nina majirani ambao kila mara wananisukuma nijiunge na siasa, lakini bado nafakiria juu suala hilo. Huwezi jua, siku moja naweza kuwa mbunge,”

King Saha ambaye anagombea wadhfa wa urais katika chama cha wanamuziki nchini uganda UMA huenda anatumia fursa hiyo kujenga misingi yake ya kisiasa ya siku za usoni.

Utakumbuka baada ya Bobi Wine kufanya makubwa katika ulingo wa siasa, wanamuziki wengi kutoka Uganda wamekuwa wakijaribu kufuata nyayo zake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke