Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amefunguka sababu za kundi la Goodlife Crew kushindwa kurudi kwenye muziki licha ya mashabiki kushinikiza achukue nafasi ya marehemu, Mozey Radio.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni King Saha amesema licha ya kufanya majaribio ya kufufua kundi hilo kwa kuachia ngoma mbili na member wa Goodlife, Weasel Manizo imekuwa vigumu kwao kufanya kazi pamoja kutokana na kila mmoja kushikika na shughuli zake za kimuziki.
King saha ambaye anafanya poa na ngoma yake iitwayo Sivaawo amesema jambo hilo limesambaratisha juhudi ya kuirudisha kundi la Goodlife Crew kwenye ramani ya muziki Afrika Mashariki, hivyo wamekubaliana na Weasel Manizo kwamba watakuwa wanaachia ngoma pindi tu mashabiki watakapohitajia.
Utakumbuka baada ya kifo cha MozeyR mwaka wa 2018 mashabiki wengi wa muziki nchini Uganda walimtaka King Saha achukue nafasi ya radio,kwenye kundi la Goodlife ambapo tuliona King Saha akifanya nyimbo mbili pamoja na Weasel, ambazo ni Mpa Love na Tubikole kama njia ya kujaribu kufufua kundi hilo.
Licha ya Nyimbo hizo kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wawili hao wamekuwa kwenye harakati zake za kufanya muziki kama wasanii wa kujitegemea