You are currently viewing KING SAHA AMJIBU BEBE COOL KWA KEJELI BAADA YA KUPINGA AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

KING SAHA AMJIBU BEBE COOL KWA KEJELI BAADA YA KUPINGA AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amejibu madai yaliyoibuliwa na Bebe Cool kuwa hana vigezo vya kuuongoza muungano wa wasanii nchini humo kutokana na kuathirika pakubwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Kupitia mitandao yake ya kijamii King Saha ameshare video ya Bebe Cool akimzungumzia vibaya na kuweka caption ya kumshukuru kwa kejeli huku akisema kwamba endapo atachaguliwa kama rais wa muungano wa wasanii nchini Uganda atamhudumia msanii huyo bila ubaguzi licha ya kumpinga vikali kwenye azma yake ya kuwa kiongozi wa wasanii.

King saha ambaye juzi kati alitangaza kuwania wadhfa wa urais kwenye muungano wa wanamuziki nchini uganda anatarajiwa kuchuana na rais wa sasa wa muungano huo Cindy Sanyu kwenye uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya ambao utafanyika hivi karibuni.

Tayari aliyekuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda Ykee Benda ameunga mkono azma ya King Saha kuwa rais wa muungano huo kwa kusema kwamba anastahili wadhfa huo licha ya kutokuwa maadili mema kama baadhi ya watu wanavyosema mitandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke