Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha ameibuka na kumtuhumu msanii mwenzake Bebe Cool kuwa nii mshirikina.
Katika perfomance yake juzi kati King Saha amesema Bebe Cool amekuwa akitumia uchawi kuwashusha wasanii wengine.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema hatua ya Bebe Cool kutumia nguvu za giza ni kwa ajili ya kubaki kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda bila kuchuja.
Utakumbuka King Saha amekuwa akirushiana maneno makali na Bebe Cool tangu bosi huyo wa Gagamel amshauri aachane na matumizi ya dawa za kulevya mwaka wa 2021.