You are currently viewing KING SAHA APINGA UCHAGUZI WA CHAMA CHA UMA KUFANYWA KWA NJIA YA KIDIJITALI.

KING SAHA APINGA UCHAGUZI WA CHAMA CHA UMA KUFANYWA KWA NJIA YA KIDIJITALI.

Mwanamuziki King Saha amepinga uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA kufanyika kwa njia ya kidijitali.

Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema uchaguzi wa chama hicho unapaswa kufanya kwa njia ya kupiga foleni kwenye vituo vya kupigia kura ikizingatiwa kuwa kanuni za kudhibiti msambao wa virusi vya covid-19 zilisitishwa a na serikali.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema kuwa huenda uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda hukakumbwa na dosari nyingi ikizingatiwa kuwa sajili ya wapiga kura aliyopewa juzi kati haina baadhi ya majina ya wasanii watakaoshiriki uchaguzi  wa chama hicho.

Hata hivyo amesema licha ya zoezi la kuwasajili wapigari kura kukamilika wiki 3 zilizopita baado mchakato wa kuwaandikisha  wasanii unaoendesha nyuma ya pazia kitu ambacho amedai huenda ni njema ya Cindy na timu yake kumuibia kura.

Utakumbuka uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA utafanyika Mei 23 mwaka huu ambaopo King Saha anatarajiwa kumenyana na rais wa sasa wa chama hicho Cindy Sanyu

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke