Msanii kutoka King Saha ameripotiwa kulazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali moja nchini nchini Uganda.
Hii ni baada ya picha yake kusambaa mtandaoni zikimuonesha akiwa kwenye kitanda cha hospitali akiipambania afya yake.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uganda, chanzo cha ugonjwa wake haijawekwa wazi ila mashabiki wanaendelea kumtumia salamu za pole apate afueni ya haraka.
Ikumbukwe Juzi kati King Saha aligonga vichwa vya habari nchini Uganda baada ya mtangazaji wa radio Brian Mulondo kumtolea uvivu, akimtaka azingatie masuala ya usafi kutokana na harufu mbaya anayotoa mwilini mwake.
Ni madai ambayo yalikaririwa na Bebe Cool ambaye alidai kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akitoa wito kwa vyombo vya habari kuungana naye kwenye kampeini ya kubadili maisha ya King Saha ambaye kwa mujibu wake ni mraibu wa dawa za kulevya.