Mwanamuziki King Saha, ambaye anatajwa kuwa Rais ajaye wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda (UMA) ametoa rai kwa msanii mwenzake Bebe Cool kumuunga mkono kwenye azma ya kuwa rais wa wasanii nchini humo kwa sababu ni amekuwa mtu mwema katika jamii.
Katika mahojiano na MwanaYouTube mmoja nchini uganda, King Saha ameelezea maisha yake yamebadilika kwa miaka ya hivi karibuni na, yuko tayari kuongoza na kutetea maslahi ya wasanii kupitia chama cha UMA.
Mwimbaji huyo amefichua kuwa hajazungumza na Bebe Cool kwa muda mrefu ila anataka wafanye kazi pamoja kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini uganda.
King Saha amesema Bebe Cool atakuwa balozi wa kumaliza matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana iwapo atashinda uchaguzi ujao wa chama cha wanamuziki nchini uganda.
Utakumbuka Bebe Cool juzi kati alipinga azma ya King Saha kuwa rais wa chama cha wasanii chini Uganda kwa kuwa msanii huyo amekuwa akitumia mihadarati na hivyo hana vigezo vya kuwaongoza wasanii.