You are currently viewing KING SAHA KUMCHAGUA BEBE COOL KUWA MSHAURI WAKE UMA

KING SAHA KUMCHAGUA BEBE COOL KUWA MSHAURI WAKE UMA

Msanii nyota nchini Uganda King Saha amedai kwamba atamchagua Bebe Cool kuwa mshauri wake pindi atakapochaguliwa kuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini humo.

Katika mkao na wanahabari King Saha amesema atafanya kazi na wasanii wote bila upendeleo licha ya baadhi yao kupinga azma yake ya kuwa rais wa muungano wa wasanii nchini Uganda.

Utakumbuka juzi kati Bebe cool alimponda sana king saha kwa kusema kwamba hana vigezo vya kuwaongoza wasanii kutokana na kuathirika na uraibu wa dawa za kulevya.

Mapema wiki hii King saha aliidhinishwa kuwa mmoja wa wagombea wa urais wa muungano wa wasanii nchini Uganda ambapo anatarajiwa kuachuana na Daddy Andre pamoja na Cindy Sanyu ambaye kwa sasa ni rais wa muungano huo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke