You are currently viewing KING SAHA KUSUSIA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA

KING SAHA KUSUSIA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA

Hitmaker wa ngoma ya “Zakayo”, Msanii King Saha amehapa kususia uchaguzi wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda kama chama hicho hakitatumia mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye vituo vya kupiga kura.

Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha ameonesha kutofurahishwa na maandalizi ya uchaguzi huo kwa kusema kwamba huenda uongozi wa chama cha UMA unalenga kuiba kura.

“Covid-19 iliisha, tunaweza tumia mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye vituo vya kupiga kura. Nitaambia wafuasi wangu wasusie uchaguzi kama utafanyika kwa njia ya SMS”, Alisema kwenye mahojiano yake

Uchaguzi wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu Mei 23 kwa njia ya SMS ambapo wapiga kura watatumia namba maalum kumpigia kura mgombea wa chaguo lao.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke