You are currently viewing KING SAHA MBIONI KUFUNGA NDOA MBELE YA HASIMU WAKE BEBE COOL

KING SAHA MBIONI KUFUNGA NDOA MBELE YA HASIMU WAKE BEBE COOL

Inaonekana Ugomvi wanamuziki King Saha na Bebe Cool kutoka uganda hautamalizika hivi karibuni.

Hii ni baada ya king saha kuibuka na kumtolea uvivu msanii mwenzake Bebe Cool akidai atafanya harusi mbele ya msanii huyo licha ya kuwa anamzidi kiumri.

Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema ni aibu kwa mtu kama Bebe Cool kutohalalisha ndoa yake kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa ana umri mkubwa kumshinda.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema atafunga harusi hivi karibuni mara baada ya ujenzi wa nyumba yake kukamilika.

King Saha amesema licha ya kuwa ana mpango wa kuhalalisha ndoa yake hivi karibuni, hatamweka wazi mke wake kwa umma kwa faida ya amani yake ya akili.

“Bebe Cool was singing when I was in P.1. He is a very old man but stuck in the skin of a young man. I’m sure even my wedding will come before his. I will wed my wife immediately after completing my house,” Amesema King Saha

Mjengo wa kifahari wa King Saha umekamilika kwa asilimia 80 na nyumba yake hiyo ipo maeneo ya Nakawuka, katika wilaya ya Wakiso nchini Uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke