Mwanamuziki kutoka uganda King Saha amethibitisha kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa na Cindy Sanyu katika uchaguzi ujao wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda (UMA).
Akiongea katika mahojiano na YouTuber mmoja nchini uganda, King Saha ameeleza kuwa hatarajii kama kutakuwa na wizi wa kura kwa kuwa anaamini uchaguzi utakuwa wa huru na haki.
“Siasa ni mchezo, kuna kushinda na kushindwa. Nitakubali matokeo ikiwa mchakato wa uchaguzi utakuwa huru na wa haki. Lakini nina matumaini, nitashinda,” alisema katika mahojiano na YouTube mmoja nchini uganda.
King Saha anachuana na mwimbaji mwenzake Cindy Sanyu kuwania urais wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda.