You are currently viewing Kiswahili inawakwamisha wasanii wa Kenya kutusua kimataifa – Asema Otile Brown

Kiswahili inawakwamisha wasanii wa Kenya kutusua kimataifa – Asema Otile Brown

Msanii nyota nchini Otile Brown amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vinavyowakwamisha wasanii wa Kenya kufanya vizuri kimataifa ni lugha.

Katika mkao na waandishi wa habari Otile amedai kuwa endapo wasanii wa Kenya wangekuwa wanaimba kwa lugha ya kingereza basi wangekua na uwanja mkubwa wa kusikika kimataifa zaidi na kupata shows tofauti tofauti za nje ya nchi.

Hitmaker huyo wa “Run Up” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa tofauti ya muziki wa Kenya na Nigeria ni lugha pekee na ndio sababu kubwa ambayo hawawezi kushindana na wasanii kutoka taifa hilo la Afrika Magharibi.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii nchini kuanza kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao ili muziki wa Kenya uweze kufika mbali zaidi.

Utakumbuka Otile Brown amekuwa nchini Marekani kwa miezi miwili ambako amekuwa akifanya shows kwenye miji mbali mbali nchini humo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke