Kiungo wa Ujerumani na Real Madrid Toni Kroos ameongezeka kwenye orodha ya wanaokosoa ushindi wa nyota wa PSG Lionel Messi ambaye usiku wa kuamkia leo aliibuka mshindi wa Tuzo ya Ballon D’Or 2021 kwa mara ya Saba kama mchezaji bora wa mwaka.
Toni Kroos amekosoa uamuzi huo kwa kusema Messi hakustahili lakini pia alihoji kwanini Karim Benzema hakushinda tuzo hiyo wakati alikuwa na msimu mzuri. “Why didn’t Benzema win the Ballon d’Or? What fails, above all, is the selection of first choice,” alihoji Toni Kroos.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 aliendelea kwa kusema hakuna shaka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekuwa wachezaji bora katika kipindi chote cha miaka 10 lakini mwaka huu ilibidi tuzo iende kwa mshambuliaji mwingine.