Mwanamuziki Kizz Daniel ametangaza kuwa atatumbuiza wimbo wake maarufu “BUGA” kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Hii ilikuwa ni ndoto ya Kizz Daniel tangu mwezi Juni mwaka huu ambapo kupitia Twitter, alianika wazi maombi yake akimuomba Mungu amsaidie kutimiza ndoto hiyo.
Lakini pia Mwanamuziki huyo wa Nigeria ametangaza rasmi Jina la Album yake mpya, ameipa Jina la (Alcohol and Cigarettes) ambayo pia itafuatiwa na Ziara ya Muziki mwaka 2023 ambayo itakwenda kwa Jina hilo hilo.